MY TIME

KIPENGELE CHA FANI KATIKA KUHAKIKI SHAIRI

Katika kuhakiki shairi ni lazima tuzingatie vipengele vya fani na maudhui.

FANI
Uhakiki wa fani katika ushairi ni uchambuzi wa kina na kuziweka wazi mbinu za kisanaa alizotumia mshairi katika kutunga kazi yake.Vipengele muhimu vya kuzingatia katika fani ya mshairi ni kama vifuatavyo:

Muundo
Katika kuhakiki muundo wa shairi , mhakiki anatakiwa aweke wazi mambo yafuatayo:
Idadi ya beti , mfano katika kuangalia  shairi letu tunaona kuwa shairi letu lina jumlaya beti tatu. Idadi na mpangilio wa vina mizani. Mfano katika shairi letu tunaona kuwa limepangwa kwa mpangilio wa vina na mizani. Mfano shairi letu lina idadi ya mizani 16, mfano

                        Ku\pi\ma\a\fya\ze\tu\ , ni\bu\re\kwa\wa\hu\si\ka\.
Pia katika shairi hili mpangilio wa vina katika ubeti wa kwanza ni sha ,a na na ubeti wa pili ni etu, ka.

Mtindo
Jambo la kuonyesha hapa ni kuonyesha iwapo shairi ni lakimapokeo au kimamboleo. Mfano          katika  kipengele hiki tunaona  kuwa shairi letu ni lakimapokeo kwa sababu ya urari wa vina na    mizani.
  
Matumizi ya lugha.
Katika kipengele hiki mhakiki huchunguza tamathali za semi, mfano tashbiha , tashhisi sitiari n.k. pamoja na lugha picha. Mfano Mstari wa pili katika shairi letu unasema “Mheshimiwa kapasha” Hapo tunaona matumizi ya msimu kapasha, mhakiki anapaswa kujiuliza kama matumzi ya lugha yamesaidia kufanikisha kufikisha ujumbe au yamefikisha shairi hilo.

No comments:

Post a Comment