MY TIME

VIPENGELE VYA MAUDHUI KATIKA KUHAKIKI SHAIRI

MAUDHUI
Ili kuhakiki na kupata maudhui ya shairi inatakiwa kulisoma shairi kwa kulielewa zaidi. Baada ya  kupata picha fulani kuhusu shairi na kutafakari maana za maneno muhimu, itatubidi tuchunguze vipengele vya maudhui ambavyo ni dhamira, ujumbe na maadili.

  a   Dhamira. Hapa kinachozingatiwa  ni malengo ya jumla ya mtunzi. Mhakiki anapaswa kubaini kubaini malengo hayo na kutathmini umuhimu wake katika jamii inayohusika. Mfano  katika shairi hili dhamira ya mtunzi ni kuhamasidha watu wapime afya zao. Mhakiki anapaswa kujiuliza dhamira hii ina umuhimu kwa Tanzania ya leo?
b  Ujumbe wa mtunzi. Mhakiki baada ya kusoma shairi lolote  anapaswa kujua na kujiuliza amepata ujumbe gani baadaya kusoma  shairi hilo. Mfano katika shairi lililopita ujumbe tulioupata katika shairi hilo ni umuhimu wa kupima afya zetu.

c    Maadili. Katika ujumbe kunaweza kuwa na maadili fulani yanayofundishwa kwa wasikilizaj au wasomaji. Mafunzo hayo yanaweza kuwa ya maadili lakini pia mapotosho kulingana na jamii husika. Mfano, maadili ya jamii fulani ni pamoja na watu wazima kuogelea wakiwa na watoto wa jinsia tofauti, lakini ikiwa kuogelea huko ni watu kuvaa nguo chache na za mbano, utaratibu huu sio maadili kwa watanzania bali ni mapotosho.

No comments:

Post a Comment