MY TIME

MAANA YA UHAKIKI

NINI MAANA YA UHAKIKI ?
Uhakiki ni kitendo cha kuchambua kazi ya fasihi , kifani na kimaudhui ili kupata ujumbe uliomo katika kazi hiyo. Kitendo hiki huweka wazi mambo ya msingi yaliyojitokeza katika kazi ya kifasihi kwa kuangalia vipengele vikuu viwili, ambavyo ni fani na maudhui.

Kuhakiki kazi ya fasihi hutuwezesha kufahamu , ubora na udhaifu wa kazi ya fasihi , uhusiano na uwiano wake na jamii inayohusika .

Wakati wa kuhakiki kazi ya kifasihi ni vizuri kujiuliza maswali yafuatayo :

1.      Baada kusikiliza kazi ya kifasihi umepata ujumbe gani?

2.      Ujumbe ulioupata ni wa kweli na unalingana na jamii inayohusika ?

3.      Je, kuna maadili au mafunzo yoyote yaliyopatikana baada ya kusikiliza kazi hiyo?

4.      Ni lugha ya namna gani imetumika kufikisha ujumbe kwa hadhira?

5.      Mtiririko wa visa na matukio ukoje?
Katika mada hii tutajifunza kuhakiki ushairi katika fasihi simulizi na kuhakiki maigizo.

No comments:

Post a Comment