MY TIME

MFANO WA SHAIRI


UHAKIKI WA USHAIRI
Ushairi ni tungo zenye kutumia mapigo ya silabi kwa utaratibu maalumu wa kimuziki kwa kutumia lugha ya mkato,lugha ya picha na tamathali za semi.  
     Mashairi ni kama kazi nyengine za kifasihi huhakikiwa kwa kutumia vigezo sawa na vinavyotumika katika kazi nyengine za kifasihi. Vigezo hivyo ni kwa kuzingatia vipengele vyake viwili yaani fani na maudhui.

MFANO WA SHAIRI
Kampeni kaanzisha , ni raisi mtutukutu,
Mheshimiwa kapasha , kupima pasi mashaka,
Kikwete alianzisha , kampeni kwa hakika,
Tupime afya zetu , Jamani tusizembee.

Kupima hiari yetu , ni bure kwa wahusika,
Na katika lengo letu , ni wote tuweze fika,
Katika vituo vyetu , majumbani tuweze toka,
Tupime afya zetu , jamani tusizembee.

Kujua afya muhimu , tutaweza adilika,
Tukapime zetu damu , kama si waathirika,
Tutapanga majukumu , malengo tuloyaweka,
Tupime afya zetu, jamani tusizembee.

No comments:

Post a Comment