MY TIME

VIPENGELE VYA FANI KATIKA KUHAKIKI MAIGIZO

FANI
Uhakiki wa fani katika maigizo unajihusisha na ufundi uliotumiwa , ufundi huu unajumuisha mambo kadhaa kama ifuatavyo:

Mtindo
Mtindo ni sura ya maigizo inayojitokeza kupitia mpangilio wa maneno na vitendo. Inabidi mhakiki achunguze kama ni mchezo wa jukwaani, majigambo, vichekesho,mazungumzo au ngonjera. Pamoja na haya mtindo hutegemea lengo la maigizo ambalo linaweza kuwa ni kuelimisha, kuburudisha au kuonya.

Wahusika
Hapa mhakiki anajiuliza ,mhusika huyu anahalisika (fanani), kweli mtu kama huyu anaweza kuonekana katika amzingira halisi yaliyotajwa.
Matumizi ya lugha.
Kama tulivyokwisha elezea katika ushairi , vile vile katika maigizo tunaangalia uteuzi wa misemo  tamathali za semi, n.k. Ikumbukwe kuwa hapa kinachotakiwa si lugha sanifu, kinachotakiwa ni uahlisia wa matumizi ya maneno hayo katika muktadha inayohusika. Fanani halazimiki kutumia lugha sanifu, anaweza kutumia lahaja, rejista na hata misimu kulingana na mazingira ya igizo.

Mandhari
Hapa mhakiki anajiuliza, je? Sura ya hapo panapofanyiwa igizo inalingana na uhalisia? Kama igizo linaakisi mazingira ya Dodoma, halafu mtunzi ameweka mandhari yenye misitu na yenye barafu, hadhira inaweza kuchanganyikiwa. Hali kama hii haitowi picha halisi ya mahali shughuli inapofanyika.
Migogoro
Maigizo hujikita kwenye mgongano wa mawazo mawili au zaidi yanayokinzana. Kunaweza kuwa na migogoro zaidi ya moja katika igizo moja. Mhakiki anatakiwa abaini migogoro itakayo wasilishwa na fanani.

No comments:

Post a Comment